Kuhusu ELM Group:

ELM Group inalenga kuwapa wanachama uhuru endelevu wa kiuchumi (financial freedom) kwa kua na tabia ya kuweka akiba, kutoa mikopo nafuu, ujuzi wa ujasiriamali, na kuongeza mtandao wa marafiki.

Malengo ELM Group:

 • Kuongeza idadi ya wanachama na kuhakikisha kunakuwepo na ubora wa mikopo, kuongeza akiba na hisa kwa kutoa huduma bora za kifedha
 • Kupokea zabuni mbalimbali na kuzifanyia kazi
 • Kuwa na miradi endelevu ya maendeleo
01

Sifa Za Kua Mwanachama

 • Awe na umri kuanzia miaka 18
 • Awe na akili timamu
 • Awe na chanzo halali cha kujiingizia kipato
 • Awe muaminifu na muadilifu
 • Awe tayari kufata taratibu zote za kikundi
02

Taratibu Za Kujiunga

 • Mwanachama atazaja fomu maalum ya kujiunga
 • Awe na kitambulisho cha Taifa,Kura au Passport ya kusafiria
 • Awe na picha Tatu za passport size
 • Mwanachama atatakiwa kulipa ada ya kiingilio cha shilingi 10,000/=
 • Mwanachama atatakiwa kuweka akiba kila mwezi kiasi  kisichopungua shilingi 20,000/=
 • Mwanachama atatakiwa kutoa kila mwezi ada ya  mchango wa jamii ambayo ni shilingi 5,000/=